KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 30, 2011

Wesley Sneijder ATANGAZA KUBAKIA ITALIA.

Kwa mara ya kwanza kiungo wa Inter Milan Wesley Sneijder ametoa kauli ya kutaka kubaki na klabu hiyo baada ya kuhusishwa na taarifa za kutaka kuondoka Guissepe Meaza katika kipindi hiki cha usajili.

Wesley Sneijder amesema kwa sasa anataka kufikiria namna ya kuisaidia klabu yake katika michezo ya ligi ya nchini Italia pamoja na ile ya kimataifa na katu hatopenda tena kuzungumzwa katika suala la usajili.

Amesema amezungumzwa na kuandikwa sana katika vyombo vya habari lakini anaona umefikia wakati wa kuzungumzwa ama kuandikwa kupitia klabu yake ya Inter Milan ambayo ilimsajili mwaka 2009 akitokea Real Madrid.

Kiungo huyo ambae ni raia wa nchini Uholanzi alikua katika mawindo makali ya kutaka kucheza soka nchini Uingereza, baada ya kukiri kupitia vyombo vya habari ambapo alinukuliwa akisema anaipenda ligi hiyo ambayo ni tajiri ulimwenguni kwa sasa.

Wesley Sneijder alikua katika mipango ya kutaka kusajiliwa na vilabu kutoka mjini Manchester ambapo Man utd walipigana vikumbo na mahasimu wao wakubwa Man City lakini mpango huo uliingia gizani.

Upande wa Man utd walifuta mipango ya kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 kufuatia Sir Alex Ferguson, kutangaza kutokumuhitaji kwenye kikosi chake ili hali Man city hawakutoa kauli ya kutaka kuendelea katika suala hilo.

No comments:

Post a Comment