KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 29, 2011

Wilson Palacios KUITUMIKIA STOKE CITY.

Uongozi wa Stoke City unajiandaa kumsajili kiungo kutoka nchini Honduras na klabu ya Tottenham hotspurs Wilson Palacios kwa ada ya uhamosho wa paund million 6.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27, usiku wa kuamkia hii leo alitarajiwa kufanyiwa vipimo huko Britannia Stadium, ikiwa ni sehemu ya kukamilishwa kwa mikakati ya usajili wake.

Meneja wa Spurs, Harry Redknapp alithibitisha taarifa hizo mara baada ya mtanange wa jana ambao ulishuhudia vijana wake wakikubali kisago cha mabao matano kwa moja katika uwanja wa nyumbani huko jijini London.

Hata hivyo Harry Redknapp alikanusha taarifa za kuondoka kwa mshambuliaji wake kutoka nchini Uingereza Peter Crouch, ambae pia alikua anahusishwa na taarifa za kutaka kusajiliwa na The Potters.

Wilson Palacios anaanza safari ya kuihama Tottenham Hotspurs huku akikumbukwa kwa ujio wake ndani ya klabu hiyo ambao uliigharimu Spurs Paund million 12 akitokea Wigan Atheltics aliyoihama mwezi januari mwaka 2009.

No comments:

Post a Comment