KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 9, 2011

Xavi Hernandes KUIKOSA ITALIA.

Kiungo wa mabingwa wa soka barani Ulaya Fc Barcelona Xavi Hernandes ameondolewa katika timu ya taifa ya Hispania ambayo kesho itakua mjini Bari ikichezamchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa dunia wa mwaka 2006 Italia.

Xavi Hernandes ameondolewa kikosini baada ya kushindwa kupona majeraha yanayomkabili kwa sasa, ambayo pia huenda yakamfanya ashindwe kuwajibika kwenye maandalizi ya msimu mpya wa ligi akiwa na klabu yake ya Barcelona.

Xavi Hernandes alifanyiwa vipimo jana jioni kabla ya safari ya timu ya taifa ya Hispania kuelekea nchini Italia na ikabainika hatoweza kucheza mchezo huo ambao itatumiwa kama sehemu ya maandalizi ya michezo ya kuwania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya mwezi Septemba.

Kiungo huyo anakua mchezaji wa pili kuondolewa katika kikosi cha Vicente del Bosque, baada ya beki wa pembeni wa Real Madrid Sergio Ramos, kuenguliwa kufuatia sababu za majeraha ya mgongo.

Kuenguliwa kwa Sergio Ramos, kumetoa nafasi kwa beki wa klabu ya Malaga Nacho Monreal kuitwa kikosini na huenda kaanzishwa katika mchezo wa kesho.

Nafasi ya Xavi Hernandes itazibwa na kiungo alieitwa kwa mara ya kwanza Thiago Alcantara ambapo inaaminiwa ataanya vizuri kama anavyokua kwenye klabu yake ya Barcelona.

Kiungo Andres Iniesta amesema kutarajia kuchezeshwa kwa Thiago Alcantara katika mchezo wa kesho dhidi ya timu ya taifa ya Italia, kutatoa mwanga kwa kinda huyo ambae ameanza kutambulika katika ramani ya soka ulimwenguni kufutia makubwa aliyoyafanya akiwa na timu ya taifa ya vijana ya Hispania pamoja na klabu ya Barcelona.

No comments:

Post a Comment