KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, September 10, 2011

AC MILAN WASHIKWA NYUMBANI.

Mabingwa wa soka nchini humo AC Milan usiku wa kuamkia hii leo wameanza kuteta ubingwa wao kwa matokeo ya sare dhidi ya SS Lazio katika uwanja wa San Siro.

AC Milan ambao walikua wakipewa nafasi kubwa ya kuchomoza na ushindi katika mchezo huo walilazimika kusubiri hadi katika dakika ya 33 kipindi cha kwanza pale mshambuliaji kutoka nchini Italia Antonio Cassano aliposawazisha bao la pili baada ya kuwa nyuma kwa idadi ya mabao mawili kwa moja.

SS Lazio walitangulia kuongoza kupitia kwa mshambuliaji wao mpya kutoka nchini ujerumani Miroslav Klose pamoja na mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa Djibril Cisse huku bao la kwanza la AC Milan likifungwa na mshambuliaji kutoka nchini Sweden Zlatan Ibrahimovic.

Hata hivyo AC Milan walitengeneza nafasi nyingi za kupata mabao kupitai kwa kiungo kutoka nchini Ghana Kevin-Prince Boateng ambae alisaidiana vizuri na kiungo aliesajiliwa kwa mkopo klabuni hapo akitokea Liverpool Alberto Aquilani lakini umakini mbovu ulipelekea matokeo kusalia mabao mawili kwa mawili.

No comments:

Post a Comment