KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, September 7, 2011

Alex Ferguson BADO YUPO YUPO SAAAAANA !!

Meneja wa mabingwa wa soka nchini humo Man Utd Sir Alex Ferguson amesisitiza kuwa hana mpango wa kustaafu kufundisha soka licha ya kutarajia kufikisha umri wa miaka 70 mwishoni mwa mwaka huu.

Fergie anatarajia kuhitimisha miaka 25 kama meneja wa klabu hiyo ya old Trafford itakapofika November 6 mwaka huu.

Hata hivyo tayari yapo majina ya makocha wengi waliotajwa kumrithibi mzee huyo mwenye umri wa miaka 69, lakini anasema ataendelea na kibarua chake huku akiwaacha mameneja vijana ambao wana ubora kwa sasa kama Jose Mourinho na Pep Guardiola wakiendelea kusubiri, lakini akakiri hajui ni yupi atakayerithi nafasi yake.

Katika hatua nyingine Sir Alex Ferguson amezungumzia suala la kiungo mshambuliaji kutoka nchini Uholanzi pamoja na klabu ya Inter Milan ya nchini Italia Wesley Sneijder kwa kusema ana uwezo mkubwa wa kuziba pengo la kiungo alitangaza kustahafu soka mwishoni mwa msimu uliopita Paul Scholes.

Amesema Sneijder ni mchezaji mzuri lakini hakuwa chaguo lao katika harakati za kumrithi Paul Scholes huku akiongeza kuwa viungo kama Xavi Harnandes pamoja na Andres Iniesta walikua kichwani mwake kwa ajili ya kutatua tatizo hilo.

Wakati huo huo Sir Alex Ferguson amewataka mashabiki wa soka ulimwenguni kote kutambua kwamba msimu huu kuna shughuli nzito ya kuwania ubingwa kutokana na ushindani anaotarajia kutoka katika viwabu vya jijini London pamoja na mjini Manchester.

No comments:

Post a Comment