KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, September 17, 2011

David Beckham AWANIWA UFARANSA.

Alikua meneja wa mabingwa wa soka nchini Italia AC Milan Leonardo Nascimento de Araújo ambae kwa sasa ni mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Paris St Germain ya nchini Ufaransa, ametangaza mipango ya kutaka kumsajili kiungo kutoka nchini Uingereza David Beckham.

Leonardo ametamngaza mpango huo, zikiwa zimepita siku kadhaa badaa ya klabu za QPR pamoja na Tottenham Hotspurs zote za nchini Uingereza kutangaza azma kama hiyo hatua ambayo inaonyesha ni vipi kutakavyokua na upinzani wa kumsajili David Beckham ambae mwezi November anamaliza mkataba wake na klabu ya Los Angel Galax ya nchini marekani.

Amesema mpango wa kumsajili kiungo huyo tayari umeshaanza kusukwa huko Parc des Princes, na anaamini mchezaji huyo atapendezwa na mazingira ya Paris St Germain ambayo kwa sasa imejizatiti kwa ajili ya kuleta changamoto mpya katika soka la nchini Ufaransa.

Leonardo ambae pai aliwahi kuitumikia Paris St Germain 1996–1997, ameendelea kubainishwa kwamba Anamfahamu vilivyo David Beckham, baada ya kumfundisha akiwa na klabu ya Ac Milan misimu miwili iliyopita hivyo atatumia nafasi hiyo kumshawishi ili ajiunge nao mwezi januari mwaka 2012.


Amesema wakati akimfundisha kiungo huyo mwenye umri wa miaka 36, alifurahishwa na mpangilio wa maisha yake ya ndani na nje ya uwanja kwani hakuna hata siku moja ambayo alikwenda kinyume na taratibu za klabu ya Ac Milan ambayo ilimsajili kwa mkopo.

Paris St Germain kwa sasa imekua miongoni mwa klabu tajiri barani ulaya baada ya kuwa chini ya muwekezaji kutoka nchini Qatar ambae anamiliki kampuni ya uwekezaji iitwayo Qatar Sports Investments.

Kufuatia hatua hiyo Paris St Germain ilifanya usajili wa wachezaji wenye majina na wenye uzoefu katika kipindi cha usajili kilichomalizika usiku wa septemba mosi na tayari usajili huo uliofanywa umeshaanza kuonyesha muelekeo wa mafanikio katika ligi daraja la kwanza nchini Ufaransa.

No comments:

Post a Comment