KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, September 13, 2011

ARSENAL KUREJEA DIMBANI HII LEO.

Washika bunduku wa Ashburon Grove Arsenal baada ya kupata ushindi wao wa kwanza katika ligi ya nchini Uingereza mwishoni mwa juma lililopita usiku huu watakua wanasaka namna ya kuendeleza furaha yao kwa kucheza na mabingwa wa soka nchini Ujerumani Borusia Dortmund.

Arsenal wamefunga safari hadi nchini humo bila ya kuwa na kiungo kutoka nchini Wales Aaron Ramsey, beki kutoka nchini Ubelgiji Thomas Vermaelen kiungo kutoka jamuhuri ya Czech Tomas Rosicky pamoja na kiungo kutoka nchini Uingereza Jack Wilshere ambao wote ni majeruhi.

Arsene Wenger meneja wa klabu hiyo ya jijini London ambae hatokuwepo katika benchi usiku huu, amesema hakuna watakachokifanya katika mpambano huo dhidi ya Borusia Dortmund zaidi ya kuangalia namna ya kupata ushindi ugenini.

Amesema anaamini ushindi wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Swansea city umewatengenezea mazingira mazuri wachezaji wake ambao pia watafurahishwa na hatua ya kurejea kwa Alexender Song pamoja na winga Gervinho.

Kwa upande wa Borusia Dortmund watamkosa Julian Koch anaesumbuliwa na maumivu ya goti Lucas Barrios anaesumbuliwa na maumivu ya misuli ya paja huku Marvin Bakalorz pamoja na Patrick Owomoyela wakitarajiwa kuwa nje pia.

Michezo mingine ya ligi ya mabingwa barani ulaya itakayochezwa usiku huu ni;


Cristal Arena, UIbelgiji
Racing Genk v Valencia CF

Stadio Karaiskaki, Ugiriki
Olympiacos v Olympique Marseille

Estádio do Dragão, Ureno
FC Porto v Shakhtar Donetsk

GSP-Stadion, Nicosia, Cyprus
APOEL Nicosia v Zenit St. Petersburg


Stadion mesta Plzne, Jamuhuri Ya Czech
Viktoria Plzen v BATE Borisov

No comments:

Post a Comment