KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, September 9, 2011

Arsene Wenger BHADO YUPO KIKAANGONI !!

Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger ameendelea kukalia kuti kavu kufuatia utafiti uliofanywa na mtandao wa YouGov kwa kuwashirikisha mashabiki wa soka ulimwenguni kote.

Utafiti huo umeonyesha kwamba Arsene Wenger bado anaendelea kupewa nafasi kubwa ya kuwa meneja wa kwanza kupoteza kiti chake miongoni mwa mameneja wanaofundiosha vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya soka nchini Uingereza msimu huu ulioanza August 13 mwaka huu.

Mashabiki 8000, waliopiga kura kupitia mtandao huo wameonyesha kutoridhishwa na ufundishaji wa meneja huyo alijiunga na Arsenal mwaka 1996, hasa ukizingatia kikosi chake mpaka sasa kimeshajikusanyia point moja baada ya kushuka dimbani mara tatu.

Pia kura hizo zinaonyesha kupigwa kwa wingi, kufuatia mashabiki hao kuonyesha kuchukizwa na matokeo mabovu ya mabao manene kwa mawili yaliyopatikana katika mchezo uliopita ambapo Arsenal waliaibishwa ugenini dhidi ya Man utd.

Katika mchanganuo wa utafiti unaofanywa na mtandao YouGov kati ya mashabiki kumi, mashabiki wawili ndio waliomuunga mkono Arsene Wenger kwa madai ya kutaka abaki kuifundisha klabu ya Arsenal.

Utafiti huo pia unaonyesha kwamba meneja wa pili anaepewa nafasi kubwa ya kutimuliwa kazi msimu huu ni meneja wa klabu ya Sunderland Steve Bruce akifuatiwa na meneja wa Bluckburn Rovers Steve kean.

No comments:

Post a Comment