KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, September 15, 2011

BABU AMKUBALI MCHEZAJI MKONGWE MAN UTD.

Winga kutoka nchini Wales Ryan Giggs amepongezwa vilivyo na meneja wa Man Utd Sir Alexander Chapman "Alex" Ferguson kufutia shughuli nzito aliyoifanya usiku wa kuamki hii leo huko mjini Lisbon katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Sport Lisboa Benfica.

Sir Alexander Chapman "Alex" Ferguson ametoa sifa hizo kwa kusema shughuli aliyoifanya winga hiyo ilikua nzuri na mwisho wa siku ilikisaidia kikosi chake kupata point moja ugenini ambayo pia amedai ni nzuri kwa upande mmoja ama mwingine.

Amesema mbali na kufunga bao la kusawazisha katika mpambano huo bado Ryan Giggs alionyesha uwezo mkubwa dhidi ya wapinzani hatua ambayo anadhani itaendelea kumjenga katika mazingira mazuri ya kuitetea Man utd msimu huu.

Katika hatua nyingine babu huyo mwenye umri wa miaka 69, ametoa pongezi kwa Ryan Giggs kufautai rekodi aliyoiweka ya kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa aliefunga bao katika michuano hiyo ambayo ni muhimu katika ngazi ya vilabu barani ulaya.

Ryan Giggs ameweka rekodi hiyo na kuivunja ile iliyowekwa na mshambuliaji mkongwe kutoka nchini Italia pamoja na klabu ya Ac Milan Filippo Inzaghi ambae kwa mara ya mwisho alipachika bao katika michuano hiyo msimu uliopita akiwa na umri wa miaka 36 na miezi sita.

Wakati huo huo Sir Alexander Chapman "Alex" Ferguson amekiri kwamba Sport Lisboa Benfica wana kikosi kizuri na ana mashaka huenda wakasumbua katika michezo ya kundi tatu ambalo linaijumuisha Man Utd, FC Basel pamoja na Otelul Galati.

No comments:

Post a Comment