KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, September 10, 2011

CAF WAWACHINJIA BAHARINI Fenerbahce.

Mahakama ya kimichezo iliyo chini ya shirikisho la soka ulimwenguni kote FIFA CAS, imetupilia mbali kesi ya mabingwa wa soka nchini Uturuki Fenerbahce ambayo ililenga kulishitaki shirikisho la soka barani ulaya UEFA, baada ya kuiengua klabu hiyo katika michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu.

CAS wametupilia mbali madai ya klabu hiyo kutokana na kushindwa kupata uhakika halisi wa malalamiko ya klabu ya Fenerbahce kutoka kwenye shiriksiho la soka nchini Uturuki ambalo tayari lilikua limeshatangaza kutowapa ushirikiano viongozi wa klabu hiyo.

Taarifa iliyotolewa na mahakama hiyo imedai kwamba malalamiko ya Fenerbahce yangesikilizwa na maamuzi kutolewa endapo shirikisho la soka nchini Uturuki lingewasilisha uthibitisho wa madai ya kuonewa na shirikisho la soka barani UEFA baada ya kuenguliwa kwa wawakilishi wao katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu huu.

Kwa mantiki hiyo sasa washindi wa pili wa ligi kuu ya soka nchini Uturuki Trabzonspor, wanaendelea kuwashiwa taa ya kijani ambayo inawawezesha kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya ambapo watafungua michuano hiyo katika hatua ya makundi dhidi ya Inter Milan siku ya jumatano ya juma lijalo.

Shirikisho la soka barani ulaya UEFA lililazimika kuiengua Fenerbahce katika michuano ya ligi ya mabingw barani Ulaya kufutia tyhuma za kujipatia ubingwa katika mazingira ya rushwa, hatua mbayo ilisababishwa zaidi ya wachezaji 30 pamoja na raisi wa klabu hiyo Aziz Yildirim, kuwekwa kizuizini na jeshi la polisi nchini Uturuki.

No comments:

Post a Comment