KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, September 3, 2011

Carlos Tevez AKIRI KUMALIZA BIFU LAKE LA MANCINI.

Mshambuliaji kutoka nchini humo Carlos Tevez ametangaza kuzika tofauti zake dhidi ya meneja wa klabu ya Man city Roberto Mancini huku akieleza wazi kuwa tayari kuitumikia klabu hiyo kwa moyo mkunjufu kama ilivyokua zamani.

Carlos Tevez, ametangaza mpango huo akiwa nyumbani kwao Argentina alipokwenda kupumzika kwa ajili ya kupisha wiki ya michezo ya kimataifa ambayo itamalizika juma lijalo.

Akiwa mjini Buenos Aires baada ya kuachwa katika kikosi cha Argentina ambacho siku ya ijumaa kilichomoza na ushindi wa bao moja kwa sifuri katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya Venezulea, mshambuliaji huyo amesema tayari wameshaketi chini na Roberto Mancini na wameelewana kwa asilimia 100.

Amesema katika mazungumzo hayo kila mmoja alikiri kwa kile alichomkosea mwenzake, hivyo kwa sasa kilicho mbele yake ni kuhakikisha Man city inatimiza malengo yaliyowekwa ya kutwaa zaidi ya ubingwa wa kombe la FA walioupata msimu uliopita.

Katika hatua nyingine Carlos Tevez, ametanabai kwamba, mazungumzo hayo pia yalipelekea kupewa ruhusa na kupumzika kama ilivyo kwa wachezaji wengine walioitwa katika vikosi vya timu zao za taifa na muda wake wa kupumzika utakapomalizika atarejea mara moja mazoezini huko nchini Uingereza.

Kama itakumbukwa vyema msimu uliopita mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, mara kadhaa alikwaruzana na Roberto Mancini kwa madai ya kupishana kauli na pengine alidai anaonewa na meneja huyo aliechukua sehemu ya Mark Hughes mwezi oktoba mwaka 2009.

Hatua hiyo ilizusha tafrani ambayo ilipelekea Carlos Tevez kutaka kundoka klabuni hapo na alibakiza asilimia ndogo kujiunga na Club Corinthias Paulista ya nchini Brazil mwishoni mwa mwezi July.

No comments:

Post a Comment