KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, September 9, 2011

Carlos Tevez KUREJESHWA KIKOSINI.

Mshambuliaji kutoka nchini Argentina Carlos Tevez kesho anatarajia kuanzishwa katika kikosi cha kwanza cha Man city, baada ya purukushani za kutaka kuihama klabu hiyo kwa kisingizio cha kuhitaji kuwa karibu na familia yake.

Carlos Tevez anapewa nafasi kubwa ya kujumuishwa katika kikoso cha kwanza hiyo kesho baada ya meneja wa Man City Roberto Mancini kukiri kwamba, mshambuliaji huyo yupo fit kufuatia kumpa nafasi ya kwenda kupumzika nyumbani kwao Argentina wakati wa michezo ya kimataifa.

Mancini amesema baada ya kurejea klabuni hapo Carlos Tevez alianza mazoezi sanjari na wachezaji wengine na ameonyesha moyo wa kujituma kama ilivyokua zamani hatua ambayo anaamini imemjengea mazinigira mazuri ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

Katika hatua nyingine Mancini amesema kiungo kutoka nchini Ufaransa Samir Nasri huenda akaitumikia Man City hiyo kesho licha ya kuvunjika kidole cha mkono wake wa kulia akiwa na timu ya taifa katika mchezo ya kuwani nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya Ulaya dhidi ya Romania siku ya jumatano.

Amesema kiungo huyo yupo vizuri na ameonyesha nia ya kutaka kucheza katika mchezo wa kesho dhidi ya Wigan Athletics na alipozungumza nae amemueleza kwamba yeye sio kipa hivyo litakua jambo la msingi akimshirikisha katika kikosi chake.

Wakati huo huo mtendaji mkuu wa Man city Garry Cook ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo baada ya kashfa ya kukebeki mama mzazi wa beki wa klabu hiyo Nedum Onuoha kwa njia tya barua pepe.

No comments:

Post a Comment