KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, September 5, 2011

Darren Barr Fletcher AWATULIZA WACHEZAJI WENZAKE.


Kiungo wa mabingwa wa soka nchini Ungereza Manchester utd Darren Barr Fletcher amewataka wachezaji wa timu ya taifa ya ya nchi hiyo kusahau yaliyopita na kutazama mchezo ujao ambao utawakutanisha na timu ya taifa ya Lithuania katika harakati za kusaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya Ulaya za mwaka 2012.

Darren Barr Fletcher ametoa rai hiyo kwa wachezaji wenzake baada ya simanzi iliyotawala katika mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita ambao ulishuhudia wakilazimishwa sare ya mabao amwili kwa mawili nyumbani dhidi ya timu ya Jamuhuri ya Czech.

Amesema bado wana nafasi ya kufanya vizuri ambapo mpaka sasa msimamo wa kundi la tisa unaonesha tofauti ya point tano zilizopo kati yao, na timu ya taifa ya jamuhuri ya Czech sio mkubwa hasa ukizaingatia bado wana michezo mitatu iliyosalia.

Katika hatua nyingine kiungo wa majogoo wa jiji Liverpool Charlie Adam, hatojumuishwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Scotland hiyo kesho kufuatia maumivu makali ya hips *TAO* yanayomkabili kwa sasa.

Charlie Adam, alipatwa na maumivu hayo mwishoni mwa juma lililopita katika mchezo wa kundi la tisa wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya barani ulaya dhidi ya jamuhuri ya Czech, hatua ambayo ilimlazimu kutolewa nje ya uwanja katika dakika ya 80.

No comments:

Post a Comment