KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, September 8, 2011

David Beckham KUSAJILIWA NA QPR?

Meneja wa QPR Neil Warnock, amesema anawashangaa wale wanaohisi klabu hiyo huenda ikawa inatania katika suala la kutaka kumrejesha nyumbani kiungo kutoka nchini Uingereza na klabu ya Los Angel galax ya nchini Marekani David Beckham.

Warnock ametoa duku duku hilo akiwa katika mkutano na waandishi wa habari hii leo alipokua akizungumzia maandalizi kabla ya mchezo wa mwanzoni mwa juma lijalo ambapo kikosi chake kitashuka katika dimba la nyumbani kucheza na Newcastle Utd.

Neil Warnock, amesema hakuna kinachoshindikana katika harakati za kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 36, hivyo amewataka mashabiki pamoja na waandishi wa habari kusubiri na kuona ni vipi watakavyofanya usajili mwezi januari mwaka 2012.

Hata hivyo amedia kwamba mbali na David Beckham pia wana nafasi wa kuwasajili wachezaji wengine wenye uwezo mkubwa duniani.

Kama itakumbukwa vyema mwanzoni mwa juma hili Makamu mwenyekiti wa klabu hiyo iliyorejea katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza msimu huu baada ya kushuka mwaka 1996, Amit Bhatia alikanusha taarifa za kuwepo kwa mpango wa kumsajili David Beckham.

No comments:

Post a Comment