KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, September 7, 2011

Fabio Capello AKIRI KIKOSI CHAKE KINA MAPUNGUFU.

Licha ya kupata ushindi wa bao moja kwa sifuri dhidi ya timu ya taifa ya Wales usiku wa kuamkia hii leo, kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza, Fabio Capello amesema wachezaji wake hawakucheza katika kiwango cha kawaida.

Fabio Capello amesema kimtazamo wachezaji wake wote walicheza chini ya kiwango na anahisi walijawa na uoga kutokana na kucheza nyumbani mbele ya mashabiki waliokua wamefurika katika uwanja wa Wimbley.

Amesema suala hilo ni la kawaida lakini atajitahidi kuwajengea mazingira wachezaji wake ili waondokane na hofu wanapocheza nyumbani ili waweze kupata ushindi mkubwa dhidi ya wapinzani wao.

Kocha huyo kutoka nchini Italia ametabai kwamba katika mchezo dhidi ya Wales, wachezaji wake walikosa nafasi nyingi za wazi ambazo zingewasaidia kuibuka na ushindi mnono, lakini utaratibu huo ulishindikana kutoka na kile alichokieleza kuwa ni uoga.

Hata hivyo Fabio Capello, ameonyesha kuridhishwa na matokeo ya bao moja kwa sifuri yaliyopatikana ambapo amesema si haba kwani wamepata point tatu muhimu ambazo zimeisogeza timu yake karibu na fainali za mataifa ya barani Ulaya zitakazochezwa nchini Poland pamoja na Ukraine mwaka 2012.

Nae mfungaji wa bao pekee la timu ya taifa Uingereza Ashley Young amesema ulikua ni usiku mzuri kwao kutokana na subra zilizokua zimetawala kwa mashabiki ambao walitaka kuona wao kama wachezaji watafanya nini dhidi ya timu ya taifa ya Wales.

Timu ya taifa ya Uingereza inahitaji point moja ili iweze kufuzu katika fainali za mataifa ya barani ulaya za mwaka 2012, na mchezo ujao itakutana na timu ya taifa ya Montenegro, Oktoba saba mwaka huu.

WAKATI huohuo shabiki mmoja wa timu ya taifa ya Wales amekutwa amekufa baada ya kushambuliwa kabla ya mchezo dhidi timu ya taifa ya Uingereza.

Taarifa iliyotolewa na shirika la upelelezi la Scotland Yard imethibitisha kifo cha shabiki huyo wa nchini Wales mwenye umri wa miaka 44 ambapo inadaiwa alishambuliwa kichwani na mashabiki wenzake na alipoteza uhai kabla ya kufia hospitalini.

Hata hivyo bado haijafahamika kulikua na ghasia kati ya mashabiki wa Uingereza dhidi ya wale wa nchini Wales licha ya jeshi la polisi jijini London kuthibitisha kuwashikilia mashabiki wanne wa timu ya taifa ya Wales wanaoshukiwa na tukio hilo.

No comments:

Post a Comment