KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, September 5, 2011

Fenerbahce WABISHA HODI CAS KUDAI HAKI YAO.


Uongozi wa klabu ya Fenerbahce ya nchini Uturuki umefungua kesi dhidi ya shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, kwa madai ya kutotendewa haki ya kuondolewa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani humo ambayo itaendelea kutimua vumbi lake kwa kushuhudia hatua ya makundi ikianza kati kati ya juma lijalo.

Fenerbahce wamefungua kesi hiyo katika mahakama ya kimichezo iitwayo Court of Arbitration for Sport *CAS* iliyo chini ya shirikisho la soka ulimwenguni kote FIFA ambapo pia wanahitaji kulipwa sehemu ya fedha walizotarajia kuzipata katika kipindi cha maandalizi ya michuano hiyo.

Uongozi wa klabu hiyo inayotuhumiwa kupanga matokeo na kujipatia ubingwa wa nchini Uturuki kwa njia zisizo halali, umesema, kesi hiyo imefunguliwa, Sepetember mosi huko CAS na unaamini haki itatendeka na pengine watalipwa fedha hizo na kurejeshwa mashindanoni.

Soko la hisa la nchini uturuki limeonyesha kwamba Fenerbahce wamepoteza kiasi cha Euro million 45, ambacho wangekipata katika maandalizi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, hatua ambayo inawafanya kulidai shirikisho la soka barani Ulaya UEFA kufuatia hasara hiyo waliyoipata.

Shirikisho la soka barani Ulaya lilitangaza kuiondoa Fenerbahce katika michuano ya ligi ya mabingwa barani humo na nafasi hiyo ikapelekwa kwenye klabu ya Trabzonspor ambayo ilimaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ya nchini Uturuki msimu uliopita.

Sakata la upangaji wa matokeo, lilisababisha zaidi ya wachezaji 30 pamoja na raisi wa Fenerbahce Aziz Yildirim kuwekwa kizuizini na jeshi la polisi nchini humo.

Katika hatua nyingine shirikisho la soka nchini Uturuki TFF, limetangaza kujiondoa katika utaratibu wa klabu hiyo kukata rufaa ya kupinga maamuzi ya UEFA kwa kutoa taarifa iliyosomeka, hatupo pamoja nao hata kidogo.

Pia shirikisho hilo limelazimika kuahirisha tarehe yakuanza kwa ligi kuu ya soka nchini humo kwa kutaka kupisha maamuzi ya mahakama ambayo yataamuru klabu ya Fenerbahce ishushwe daraja ama kusalia katika ligi hiyo kufuatia sakata la rushwa linalowaandama.

No comments:

Post a Comment