KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, September 16, 2011

Gabriel Agbonlahor AWATAJA WABAYA WAKE.

Mshambuliaji wa klabu ya Aston Villa Gabriel Agbonlahor amemlaumu wazi wazi aliekua meneja wa klabu hiyo Gerrard Houllier kwa kusema amekua chanzo cha kushindwa kufikia malengo yake ya kucheza katika timu ya taifa ya Uingereza.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ametoa lawama hizo kwa kusema meneja huyo kutoka nchini Ufaransa alikua hampi nafasi ya kutosha ya kucheza ili hali alikua na kila sababu za kujumuishwa kikosini kama ilivyokua kwa wachezaji wengine huko Villa Park.

Amesema pamoja na kuoenakana kwa matatizo hayo bado aliekua msaidizi wa Gerrard Houllier, Gary McAllister alishindwa kumshawishi bosi wake kufanya namna yoyote ile, ili aweze kujumuika na wengine kikosioni.

Mshambuliaji huyo pia akaendelea kumlaumu Gary McAllister kwa kuendeleza kasumba ya kutokumchezesha mara baada ya kuondoka kwa Gerrard Houllier, hatua ambayo ilimsukuma na kuamini huenda ulikua ni mpango wa kumdidimiza kisoka.

Amesema miaka mitatu iliyopita tayari alianza kuonyesha namna ya kutimiza ndoto zake kwa kuitwa katika timu ya taifa ya Uingereza, lakini ndoto hizo zilififia na kuwaacha akiwana Ashley Young na Theo Walcott alioanza nao wakiendelea kuitwa kikosini hadi hivi sasa.

Gabriel Agbonlahor amechagulia kuwa mchezaji wa klabu ay Astona villa kwa mwezi uliopita kufuatia kazi nzuri aliyoifanya ya kufunga bao safi katika mchezo wa ligi dhidi ya Blackburn Rovers pamoja na kupachika bao la kusawazisha katika mchezo dhidi ya Everton.

Ligi guu ya soka nchini Uingereza kesho inaendelea tena kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja tofauti ambapo:

Ewood Park, Blackburn
Blackburn Rovers v Arsenal

Goodison Park, Liverpool
Everton v Wigan Athletic

Reebok Stadium, Bolton
Bolton Wanderers v Norwich City

Villa Park, Birmingham
Aston Villa v Newcastle United

The Liberty Stadium, Swansea
Swansea City v West Bromwich Albion

Molineux, Wolverhampton
Wolverhampton Wanderers v QPR

No comments:

Post a Comment