KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, September 12, 2011

Heurelho Gomes KUONDOKA JANUARI 2012.

Kipa kutoka nchini Brazil Heurelho Gomes amepewa ruhusa na kuondoka White Hart Lane mwezi januari mwaka 2012 baada ya mambo kumuendelea kombo kufuatia ujio wa kipa mwenye uzoefu mkubwa Brad Friedel.

Heurelho Gomes amepewa ruhusa hiyo na bosi wake Harry Redknapp ambapo amesema kwa sasa kipa huyo hana raha ya kuendelea kubaki katika utawala wake hivyo jambo la busara kumpa uhuru ili aweze kutafuta timu katika dirisha dogo la usajili.

Redknapp amedai kwamba hakuwa na lengo baya kufanya usajili wa kipa katika kipindi kilichomalizika usiku wa September mosi, ila lengo lake lilikua ni kuboresha kikosi chake ambacho msimu uliopita kilipoteza point nyingi kutokana na mapungufu ya Gomez.

Meneja huyo kutoka nchini Uingereza pia ametetea maamuzi ya kumpandisha Carlo Cudicini na kuwa kipa chaguo la pili, kwa kusena kipa huyo ana ubora zaidi kuliko Gomez, hatua Ambayo imeendelea kumpa wakati mgumu mbrazil huyo.

Mwishoni mwa juma lililopita katika mchezo wa ligi dhidi ya Wolves, Gomes hakuwepo kabisa katika kikosi kilichosafiri hadi mjini Wolverhampton kufuata point tatu muhimu.

Tottenham Hotspurs walimsajili Gomes mwenye umri wa miaka 30, mwaka 2008 kwa ada ya uhamisho wa paund million 8 akitokea katika klabu ya PSV Eindhoven ya nchini Uholanzi.

No comments:

Post a Comment