KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, September 7, 2011

ITALIA NA HISPANIA ZAKATA TIKETI ZA ULAYA 2012.


Mabingwa wa dunia wa mwaka 2006, timu ya taifa ya Italia pamoja na mabingwa wa sasa wa dunia timu ya taifa ya Hispania wamefanikiwa kukata tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya barani ulaya za mwaka 2012, baada ya michezo yao ya usiku wa kuamkia hii leo.

Italia wamefanikisha safari yao ya kuelekea nchini Poland pamoja na Ukaraine kufuatia bao pekee lililofungwa na mshambuliaji wa Inter Milan Giampaolo Pazzini dhidi ya timu ya taifa ya Slovenia.

Kufuatia ushindi huo wa bao moja kwa sifuri timu ya taifa ya Italia imefikisha point 22 ambazo zinawawezesha kuongoza kundi la tatu, wakifuatiwa na timu ya taifa ya Serbia yenye point 14.

Nao mabingwa wa dunia pamoja na mabingwa wa barani ulaya timu ya taifa ya Hispania wanaendelea na kamepni za kutetea ubingwa wao, baada ya kuibanjua timu ya taifa ya Liechtenstein mabao sita kwa sifuri.

Mabao ya Hispania katika mchezo huo yalipachikwa wavuni na Alvaro Negredo katika dakika ya 34 na 37, Xavi Hernández katika dakika ya 44, Sergio Ramos katika dakiak ya 52 pamoja na David Villa katika dakika ya 60 na 79.

Ushindi huo unaifanya timu ya taifa ya Hispania kufikisha point 18 ambazo zinawafanya kuongoza kundi la tisa, wakifuatiwa na timu ya taifa ya jamuhuri ya Czech wenye point 10.

Nchi ya Italia pamoja na Hispania zinajiunga na timu ya taifa ya Ujerumani pamoja na wenyeji wa fainali za mataifa ya barani Ulaya Poland na Ukraine ambazo zimeshajipatia tiketi ya kucheza fainali hizo.
Nao vinara katika ubora wa viwango vya soka ulimwenguni timu ya taifa ya Uholanzi, wenyewe wanahitaji point moja ili waweze kutinga katika fainali hizo, baada ya usiku wa kuamkia hii leo kupata ushindi wa mabao mawili kwa sifuri dhidi ya Finland yaliyofungwa na Kevin Strootman pamoja na Luuk de Jong.

Uholanzi wamesaliwa na michezo miwili dhidi ya Sweden pamoja na San Marino.

Nao mabingwa wa dunia wa mwaka 1998 pamoja na mabingwa wa ulaya mwaka 200 timu ya taifa ya Ufaransa wamevutwa shati, baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana dhidi ya Romania, huku Bosnia-Hercegovina wakitimiza azma ya kuwabanjua Belarus bao moja kwa sifuri.

Msimamo wa kundi nne unaonyesha kwamba timu ya taifa ya Ufaransa ipo kileleni kwa kufikisha point 17, ikifuatiwa na timu ya taifa ya Bosnia-Hercegovina yenye point 16.

No comments:

Post a Comment