KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, September 12, 2011

Joey Barton KUWA CHINI YA ULINZI USIKU WA LEO.

Meneja wa QPR Neil Warnock amesema hategemei kama kiungo Joey Barton atafanya upuuzi katika mchezo wa usiku huu ambao unakwenda kuwakutanisha na klabu yake ya zamani Newcastle Utd iliyofunga safari hadi huko Loftus Road.

Warnock amezungumza suala hilo baada ya kuulizwa na waandishi wa habari katika mkutano uliolenga kuzungumzia mchezo wa usiku huu ambapo amedai kwamba anaamini Barton atacheza soka la kawaida.

Amesema tayari ameshakaa na kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 na kumueleza madhara ambayo huenda yakampta endapo atafanya upuuzi na kupelekea hatua ya kuadhibiwa usiku huu hivyo hatarajii mambo tofauti kutoka kwake.

Hata hivyo amedai kwamba amempiga marufuku Joey Barton kutumia mtandao wa kijamiii wa Twiter mpaka mpambano wa usiku huu utakapo malizika na hii ni kutokana na kuhofia huenda angeanza kuwashambulia wachezaji pamoja na viongozi wa timu pinzani nje ya uwanja.

Mbali na kuzungumzia upande wa Barton pia Neil Warnock akazungumzia mchezo wote kwa ujumla kwa kusema utakua mgumu kwa kila upande.

Kama itakumbukwa vyema kabla ya kuuzwa katika klabu ya QPR, Joey Barton alikua na matatizo na viongozi wa Newcastkle Utd, baada ya kuusemea mbovu kupitia mtandao wa kijamii ambapo alieleza hisia zake baada ya kuchukizwa na mwenendo wa uongozi huko St James Park.

Nae meneja wa Newcastle Utd Alan Pardew amesema hakuna asiemfahamu Barton kwa tabia yake na hadhani kama ana ubaya na Newcastle Utd zaidi ya kutambua aliondoka St James Park kwa wema.

No comments:

Post a Comment