KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, September 6, 2011

JOSEPH YOBO AREJESHWA KWA MKOPO.

Beki kutoka nchini Nigeria Joseph Yobo amerejeshwa kwa mkopo katika klabu ya Fenerbahce ya nchini Uturuki akitikea Kwenye klabu yake ya Everton ya nchini Uingereza.

Joseph Yobo amerejeshwa kwa mkopo katika klabu hiyo baada ya kuitumikia kwa msimu uliopita ambao ulishuhudia Fenerbahce wakitwaa ubingwa wa nchini Uturuki ambao ulizua utata kufuatia sakata la upangaji wa matokeo.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 31, alipanga kuondoka Goodson Park moja kwa moja mwishoni mwa msimu uliopita, lakini mipango hiyo haikukamilika na mwishowe uongozi wa Everton ulimtaka kurejea mjini Liverpool mwezi July kwa ajili ya kuanza mazoezi sanjari na wachezaji wengine.

Hata hivyo katika hali ya mshangao Joseph Yobo ametakiwa kurejea tena kwa mkopo mjini Istanbul, hatua mbayo inaanza kuhisiwa huenda akakamilisha ndoto zake za kuihama moja kwa moja everton utakapofika mwishoni mwa msimu huu.

No comments:

Post a Comment