KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, September 16, 2011

Juan Carlos Garrido AUKATAA MTAZAMO WA MASHABIKI.

Meneja wa Villareal Juan Carlos Garrido amekataa kukubaliana na mtazamo wa mashabiki wa soka nchini humo, ambao unamuegemea kwa kusema ameonyesha kukata tamaa na matokeo mabovu ya michezo ya kwanza ya mwanzoni mwa msimu huu.

Juan Carlos Garrido ameukataa msimamo huo kwa kusema yeye bado ana mipango madhubuti ya kuiwezesha klabu hiyo kurejea katika njia za ushindi na anaamini suala hilo litawezekana kutokana na kikosi alichonacho.

Amesema kuanza vibaya mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa ligi ya nchini Hispania, kwa kufungwa mabao matano kwa kwa sifuri dhidi ya mabingwa watetezi FC Barceolona, na kisha kupata matokeo ya sare dhidi ya Sevilla kabla ya kubamizwa mabao mawili kwa sifuri dhidi ya Bayern Munich katika michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya, bado hakumsumbui hata kidogo.

Juan Carlos Garrido amedai kuwa Villareal ni kwabu kubwa na ina msimamo wake wa kipekee, hivyo bado akaendelea kusisitiza jambo la matumaini ya kukiamini kikosi chake hadi mwishoni mwa msimu huu.

No comments:

Post a Comment