KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, September 2, 2011

KAKA AFICHUA SIRI YA KUBAKI REAL MADRID.

Kiungo wa kutoka nchini Brazil na klabu ya Real Madrid Ricardo Kaka, amepasua ukweli wa kile kilichopelekea kushindwa kuondoka Estadio Stantiago Bernabeu katika kipindi cha miezi mitatu ya usajili kilichofungwa usiku wa kuamkia September mosi.

Rocardo Kaka ambae alikua anahusishwa na taarifa za kuuzwa moja kwa moja ama kupelekwa kwa mkopo katika kipindi cha usajili amesema kujiamini kwake kumemsababishia kufuta mipango ya kuihama Real Madrid katika msimu huu.

Amesema hatua ya kujiamini anapokua uwanjani na hata akiwa anazungumza na bosi wake kutoka nchini Ureno Jose Mourinho imejijengea mazingira ya kuaminiwa na kila mtu na ndio maana ilikua vigumu kuondoka na kujiunga na klabu nyingine.

Hata hivyo amedai kuwa, rayari ameshayazoea mazingira ya Real Madrid toka alipojiunga na klabu hiyo mwaka 2009 akitokea AC Milan kwa ada ya uhamisho wa paund million 61.7, hivyo lingekua jambo la kipuuzi kwake kuondoka na kwenda kusaka namna ya kuzoea sehemu nyingine.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 amedai kwamba mara kadhaa alikua anafanya mazungumzo Jose Mourinho juu ya uwezekano wa kusajiliwa na klabu zilizokuwa tayari kufanya hivyo, lakini alimuhakikishia wazi wazi kuwa yu tayari kuwania nasafi kwenye kikosi cha kwanza bila kipingamizi.

Rocardo Kaka toka alipojiunga na Real Madrid amekua na wakati mgumu wa kujihakikishia nafasi katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo kufuatia hali ya majeruhi inayomkumba mara kwa mara, hatua ambayo ilipelekea kuanza kufikiriwa huenda anahitaji muda wa kwenda kurejesha kiwango chake kwa kuuzwa kwa mkopo na pengine kuuzwa kabisa.

Katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya soka nchini Hispania uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita, Rocardo Kaka aliifanikiwa kufuinga moja ya mabao sita waliyoangushiwa Real Zaragoza.

Klabu zilizokua zinamuwania Rocardo Kaka katika kipindi cha usajili ni klabu yake ya zamani AC Milan ya nchini Italia, Arsenal pamoja na Tottenham Hotspurs zote za nchini Uingereza.

No comments:

Post a Comment