KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, September 6, 2011

Vicente del Bosque AWATWISHA MZIGO WA LAWAMA WACHEZAJI WAKE.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo, Vicente del Bosque amesema wachezaji wake wanastahili kulaumiwa kufuatia fujo zilizojitokeza katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita nchini Uswiz dhidi ya Chile.

Vicente del Bosque amepasua ukweli huo kufuatia lawama zote kuangushwa kwa wachezaji wa timu ya taifa ya Chile ambao kwa asilimia kubwa walionekana kumzonga muamuzi wa mchezo huo kila lilipotokea jambo la utata.

Amesema kwa kiasi fulani wachezaji wake walichangia fujo hizo, kwa kujibishana na wachezaji wa timu pinzani hatau ambayo haikustahili kupewa kipaumbele, hasa ikizingatiwa siku ya mchezo huo ilikua ni siku maalum ya kuuenzi mchezo wa kiungwana *Fair Play* ambao umekua unapigiwa kelele na shirikisho la soka ulimwenguni FIFA kila kukicha.

Hata hivyo amedai kwamba, kutokana na fujo zilizojitokeza katika mchezo huo, wachezaji wake pamoja na benchi zima la ufundi wamejifunza masuala mbali mbali ambayo yatawasaidia hasa katika mchezo wa hii leo wa kuwanai nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya barani ulaya dhidi ya Liechtenstein.

Katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Chile wachezaji wa timu ya taifa ya Hispania walionekana kuwa kitu kimoja pasipo kujali itikadi zao za klabu ambapo hatua hiyo iliwafurahisha wengi na kuamini huenda yale yaliyofanyika nyuma wakati wa mchezo wa Barcelona dhidi ya Real Madrid yameshafutwa.

Endapo timu ya taifa ya Hispania itachomoza na ushindi katika mchezo wa hii leo dhidi ya Liechtenstein, itaungana na timu ya taifa ya Ujerumani kwa kupata tiketi ya kushiriki fainali za mataifa ya barani ulaya za mwaka 2012 ambazo zitafanyika nchini Ukraine pamoja na Poland.

No comments:

Post a Comment