KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, September 5, 2011

Leighton Baines AMPA WAKATI MGUMU CAPELLO.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Fabio Capello, ameendelea kupata pigo katika kikosi chake, kufuatia hii leo kumpoteza beki wa pembeni wa klabu ya Everton Leighton Baines anaesumbuliw ana maumivu ya nyama za paja.

Fabio Capello amempoteza beki huyo katika kipindi muafaka ambacho kinasubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi nchini Uingereza, kwa ajili ya kutazama ni vipi watakavyofanya kweli katika mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya bara la Ulaya za mwaka 2012, dhidi Wales hapo kesho.

Leighton Baines, ameondolewa kikosini na kwa hivi sasa juhudi zinafanywa na jopo la madaktari wa klabu ya Everton, kuhakikisha anacheza mchezo wa mwishoni mwa juma hili ambapo The Toffees watakua nyumbani Goodison Park kuwakabili Aston Villa.

Kuumia kwa beki huyo kunamfanya Fabio Capello kusaka mbinu mbadala za kumpata mchezji anaecheza nafasi ya beki wa upande wa kushoto, baada ya beki mzoefu anaecheza nafasi hiyo Ashley Cole kuendelea kusumbuliwa na maumivu ya paja.

Fabio Capello pia ameshawapoteza wachezaji wengine wawili toka mwishoni mwa juma lililopita baada ya mchezo dhidi ya Builgaria ambao ni Darren Bent pamoja na Micah Richards wanaosumbuliwa na maumivu ya nyonga.

No comments:

Post a Comment