KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, September 14, 2011

MAN UTD KUANZA KAMPENI YA ULAYA HII LEO.

Michuano hiyo hii leo inaendelea tena kwa kushuhudia michezo ya kundi la kwanza hadi la nne, ambapo mabingwa wa soka nchini Uingereza Man Utd wamesafiri hadi nchini Ureno katika mji wa Lisbon, kwa ajili ya kupambana na wapinzani wao Sport Lisboa Benfica.

Man Utd wamesafiri bila ya kuwa na beki wao wa kutumainiwa Rio Ferdinand ambae ni majeruhi lakini anapewa nafasi kubwa ya kuchezeshwa katika mchezo wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Chelsea.

Man Utd pia watamkosa beki mwingine Nemanja Vidic anaesumbuliwa na maumivi ya kiazi cha mguu huku wachezaji wengine ambao hawakusafiri na timu ni pamoja na kiungo Tom Cleverley anaesumbuliw ana maumivu ya mguu toka mwishoni mwa juma lililopita, mshambuliaji Danny Welbeck anaesumbuliwa na maumivu ya nyama za paja pamoja na Rafael Da Silva anaesumbuliwa na maumivu ya bega.

Kwa upande wa Sport Lisboa Benfica huenda wakamkosa kiungo kutoka nchini Argentina Enzo Perez ambae bado yupo katika mashaka ya kucheza ama kutokucheza kufuatia maumivu ya goti yanayomkabili, huku taarifa zingine zikithibitisha kurejea kikosini kwa wachezaji kama Ezequiel Garay, Manuel Agudo Durán Nolito, Maxi Pereira pamoja na Ruben Amorim.

Meneja wa Man Utd Sir Alexander Chapman "Alex" Ferguson tayari ameshaonyesha imani ya kupata ushindi katika mpambano wa usiku huu, kufuatia kauli aliyoitoa katika mkutano na waandishi wa habari ambayo imeegemea sana katika upande wa mwanzo mzuri waliouonyesha.
Nao Man city watakuwa wenyeji wa Società Sportiva Calcio Napoli toka nchini Italia ambapo meneja wa klabu hiyo Roberto Mancini amesema siku ya hii leo, kwake anaichukua kama ni siku muhimu kwa klabu hiyo ambayo ina miaka kadhaa iliyoshuhudia wakishindwa kucheza katika michuano ya barani ulaya.

Michezo mingine ya ligi ya mabingwa barani ulaya itakayochezwa hii leo ni pamoja na;

El Madrigal, Villarreal
Villarreal CF v Bayern Munich


Stadium Lille Métropole,
Lille OSC v CSKA Moscow


Stadio Giuseppe Meazza, Milan
Internazionale v Trabzonspor


Sankt Jakob-Park, Basel
FC Basel v Otelul Galati


Amsterdam ArenA.
Ajax v Olympique Lyon


Maksimir, Zagreb
Dinamo Zagreb v Real Madrid

No comments:

Post a Comment