KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, September 8, 2011

MANCINI AFUCHUA SIRI YA KUMSAJILI OWEN.

Meneja wa Manchester City Roberto Mancini amesema sheria ya shirikisho la soka barani Ulaya UEFA ya kuzitaka klabu kutumia kama zinavyoingia mapato ya fedha, iliwasukuma kumsajili kiungo kutoka nchini Uingereza Owen Hargreaves.

Roberto Mancini ametoa sababu hiyo huku akielewa wazi kwamba walikua na mipango ya kutaka kumsajili kiungo kutoka nchini Italia na As Roma Daniele de Rossi ama kiungo kutoka nchini Argentina na Real Madrid Fernando Gago lakini waligundua wangetumia kiasi kikubwa cha fedha na kuvunja sheria za UEFA.

Amesema Gago ni mchezaji mzuri hali kadhalika Daniele de Rossi ana sifa kama hizo lakini waliona shughuli ingekua nzito kuwang’oa katika vilabu vyao vinavyowashikilia kwa sasa.

Wakati huo huo:

Manchester City huenda wakamkosa kiungo kutoka nchini Ufaransa Samir Nasri katika mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza mwishoni mwa juma hili ambapo watacheza na Wigan Atheletics.

Samir Nasri ambae alicheza kwa dakika 90 katika mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya barani ulaya mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Albania, waliokubalia kisago cha mabao mawili kwa moja, na kutumika kama mchezaji wa akiba katika mchezo dhidi ya Romania uliomalizika kwa sare ya bila kufungana siku mbili zilizopita, amevunjika mkono.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 anadaiwa kuvunjika mkono akiwa katika mchezo dhidi ya Romania, huku vyombo vingine vya habari vikieleza amavunjika kidole cha mkono wa kulia.

Mbali na kuhofiwa kukosa mchezo wa mwishoni mwa juma hili pia Samir Nasri huenda akaukosa mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya SS Napoli juma lijalo.

No comments:

Post a Comment