KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, September 12, 2011

MANCINI AWATAKA MASHABIKI KUTOITAJA BARCELONA.

Meneja wa Man City Roberto Mancini amesema ni mapema mno kukifananisha kikosi chake na mabingwa wa soka nchini Hispania pamoja na barani ulaya kwa ujumla FC Barcelona.
Mancini ametoa kauli hiyo, kufuatia mashabiki wa Man city kutamba na kukifananisha kikosi chao kama FC Barcelona kufuatia mwenendo mzuri walioa nao toka ulipoanza msimu huu wa ligi.

Mancini amesema anatambua kwa nini mshabiki hao wanathubutu kukifananisha kikosi chake kama Barcelona, lakini si kwa wakati huu ambapo yeye binafsi anaona bado sifa hiyo haijatimia kwa asilimia 100.

Amesema ni kweli mwenendo wao ni mzuri lakini, hakuna jinsi ya kujifananisha na FC Barcelona ili hali ndio mwanzo mwa msimu ambapo kwa upande wao mambo yamewaendelea vizuri na mpaka sasa wameshajikusanyia point 12.

Hata hivyo meneja huyo kutoka nchini Italia, ametoa ushauri kwa mashabiki wa Etihad Stadium kufanya jambo la subra hadi mwezi May mwaka 2012, ambapo litapatikana jibu la nani atatwaa ubingwa wa nchini Uingereza pamoja na ule wa barani Ulaya.

Katika hatua nyingine Roberto Mancini amekiri kuona ugumu katika michezo ya ligi ya mambingwa barani Ulaya ambapo kikosi chake kitafungua michuano hiyo katika hatua ya makundi kwa kucheza nyumbani dhidi ya SS Napoli hapo kesho.

Amesema michuano hiyo inashirikisha klabu kubwa na nzuri barani humo, hivyo anategemea upinzani mkubwa lakini hata hivyo akajitetea kwa kutanabai kwamba atahakikisha kikosi chake kilichosheheni wachezaji wenye uzoefu kinapigana hadi mwisho.

No comments:

Post a Comment