KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, September 7, 2011

Mark Fish AIPA UBINGWA WA MTN8 ORLANDO PIRATES.

Aliekua beki wa timu ya taifa ya Afrika kusini Mark Fish amesema Orlando Pirates wana nafasi kubwa ya kuibuka kidedea katika mchezo wa hatua ya fainali ya MTN8 ambao utawakutanisha na mahasimu wao wakubwa Kaizer Chiefs mwishoni mwa juma hili.

Fish, ambae alikua miongoni mwa wachezaji wa Bafana Bafana waliotwaa ubingwa wa barani Afrika mwaka 1994 pamoja na ubingwa wa nchini Afrika kusini mwaka 1995 akiwa na Orlando Pirates ametoa sababu za kusema hivyo ambapo ameeleza wazi kwamba Kizer Chief ni wadhaifu kuliko wapinzani wao.

Amesema amefuatilia michezo ya klabu hizo mbili toka msimu huu ulipoanza na amebaini Orlando Pirates wanacheza kwa kuelewana huku wakitengeneza mipango ya kusaka mabao zaidi ya Kaizer Chief ambao wanakosa sifa hizo.

Wakati Mark Fish akiwanyima ushindi Kaizer Chief katika mchezo huo wa mwishoni mwa juma hili, beki wa klabu hiyo Jimmy Tau amesema mchezo huo ni muhimu sana kwao hivyo watahakikisha wanacheza kufa na kupona na kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa MTN8 kwa mwaka huu wa 2011.

Amesema kwa sasa wanajiandaa vyema na mpambano huo na wanaamini maandalizi waliyoyafanya kabla ya kuanza kwa msimu wa ligi huko nchini Afrika kusini pamoja na michezo ya ligi waliyocheza mpaka sasa itawasaidia kwa kiasi kikubwa katika hatua ya kutimiza malengo ya kupata ushindi.

No comments:

Post a Comment