KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, September 3, 2011

Mesut Ozil AWATAHADHARISHA FC BARCELONA.Kiungo kutoka nchini Ujerumani Mesut Ozil amesema anaamini zama za kutesa kwa mabingwa wa soka nchini Hispania pamoja na barani Ulaya kwa ujumla FC Barcelona zimefikia tamati na sasa ni zama za klabu ya Real Madrid.

Mesut Ozil ametoa tambo hizo kwa kigezo cha kuwa na meneja mwenye uwezo wa kuteka saikolojia za wapinzani Jose Mourinho ambapo amesema hakuna litakaloshindikana dhidi ya meneja huyo katika harakati za kuzipiku mbinu za wapinzani wao.

Amesema kwa sasa Jose Mourinho amejitahidi kwa kila hali kurekebisha makosa yaliyojitokeza msimu uliopita na hadhani kama, wapinzani wao watawashinda kirahisi kama ilivyokua msimu uliopita ambao ulishuhudia FC Barcelona wakitwaa ubingwa wa LA LIGA kwa tofauti ya point nne.

Hata hivyo kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22 amesema kushindwa kwao katika mchezo wa kuwania ubingwa wa Spanish Super cup dhidi ya Fc Barcelona mwezi uliopita, kumewafunza mambo mengi wao kama wachezaji, na pia kwa meneja huyo fundisho hilo litakuwepo kwa asilimia 100.

Katika hatua nyingine Mesut Ozil amedai kwamba ukame wa kutwaa ubingwa wa LA LILA kwa misimu mitatu mfululizo unaokiandama kikosi cha Real Madrid nao unachangia kumfanya Jose Mourinho kusaka mbinu mbadala zitakazo msaidia.

Katika msimu huu wa ligi, Real Madrid tayari wameshacheza mchezo mmoja dhidi ya Real Zaragoza na walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao sita kwa sifuri ili hali FC Barcelona nao wana mchezo mmoja ambao ulimalizika kwa ushindi wa mabao matano kwa sifuri dhidi ya Villareal.

No comments:

Post a Comment