KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, September 15, 2011

Mikel Arteta ATOBOA SIRI YA KUISHI VYEMA EMIRATES STADIUM.

Kiungo kutoka nchini Hispania Mikel Arteta ametoboa siri ya kuendelea vyema na maisha ya huko Emirates Stadium mara baada ya kujiunga na Arsenal usiku wa kuamkia Septemba mosi akitokea Goodson Park yalipo makao makuu ya klabu ya Everton.

Mikel Arteta ambae mpaka sasa ameshaitumikia Arsenal katika michezo miwili amesema siri kubwa ya kufanikiwa kuishi vyema huko kaskazini mwa jiji la London ni ushauri mzuri alioupokea kutoka kwa aliekua nahodha na kiungo wa The Gunners Cesc Fabregas ambae ameamua kurejea nyumbani mjini Barcelona.

Amesema mara baada ya kujiunga na Arsenal Cesc Fabregas amekua mtu wake wa karibu na kila mara wamekua na mawasiliano na kikubwa anachomuambia ni namna ya kuishi katika mazingira ya mzee Arsene Wenger ambae amedai bado anampenda na kumuheshimu.

Amesema Fabregas alimueleza kuwa amefurahishwa na kitendo cha yeye kuhamia katika klabu ya Arsenal ambayo ilikua inamuhitaji mchezaji kama Mikael Arteta kwa kipindi kirefu.

Mbali na kueleza furaha zake kwa Mikael Arteta pia Fabregas amedai kumfundisha mipango ya kuiwezesha klabu hiyo kupata ushindi na kurejea katika makali yake kama ilivyokua zamani.

Nae kiungo kutoka nchini Israel Yossi Benayoun aliejiunga na The Gunners kwa mkopo wa muda mrefu akitokea Chelsea ameelezea furaha yake ya kuitumikia kwa moyo mkunjufu Arsenal hatua ambayo amedai imemkuna Arsene Wenger.

Amesema toka alipopewa nafasi kama mchezaji wa akiba katika mchezo wa ligi wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Swansea city waliokubali kichapo cha bao moja kwa sifuri, pamoja na mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Borusia Dortmund ambapo alicheza toka mwanzo amekua ni mwenye furaha isiyo kifani.

Wakati huo huo Yossi Benayoun ameelezea imani yake kwa kikosi cha Arsenal mara baada ya matokeo ya sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Borusia Dortmund ambapo amesema ni hatua nzuri ambayo itawawezesha kuendeleza wimbi la ushindi katika mchezo wa ligi wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Blackburn Rovers.

No comments:

Post a Comment