KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, September 5, 2011

MIMI SIO YUDA MSALITI - Raul Meireles.

Kiungo kutoka nchini Ureno Raul José Trindade Meireles ametetea maamuzi yake ya kujiunga na klabu ya Chelsea akitokea Liverpool siku ya mwisho ya dirisha la usajili huko barani Ulaya.

Raul Meireles amelazimika kuitetea nasfi yake kufuatai mashabiki wa klabu ya Liverpool kumuandama na kumuita msaliti ambae hafai hata kutazamwa machoni pale anapokua katika pirika za maisha yake.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 amesema kuondoka kwake Liverpool hakustahili kuchukuliwa kama uhasama na mashabiki wa klabu hiyo zaidi ya kuzidisha upendo kama walivyoishi siku za nyuma huko Anfield wakati akitokea FC Porto mwaka 2010 kwa ada ya uhamisho wa paund million 13.

Amesema anaumizwa na jina la yuda kila anapoona linahusishwa na uhamisho wake na anatambua jina hilo limekuja kufuatia kitendo cha kuomba uhamisho wa kuondoka Meceyside dakika za lala salama na kujiunga na Chelsea kwa ada ya uhamisho wa paund million 12.

Hata hivyo amedai kwamba Liverpool bado ni klabu nzuri na ataendelea kuipenda na daima hawezi kuizungumza vibaya, eti kwa sababu ya kuondoka kwake baada ya kuitumikia kwa kipindi cha msimu mmoja uliopita.

Kuondoka kwa Raul Meireles kunahusishwa na muonekano wa kikosi cha Liverpool kwa sasa ambacho kimesheheni wachezaji wanaocheza nafasi ya kiungo kama Jordan Henderson aliesajiliwa akitokea Sunderaland pamoja na Charlie Adam alietokea Blackpool.

Mbali na wachezaji hao bado kuna wachezaji wengine wengi wanaocheza nafasi ya kiungo ndani ya Liverpool kama Lucas Leiva, Steven Gerrard, Stewart Downing, Jay Spearing, Raheem Sterling, Jonjo Shelvey, pamoja na Conor Coady ambao pia wanahusishwa na hatua ya kuondoka kwa Meireles.

No comments:

Post a Comment