KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, September 7, 2011

Mohammed Bin Hammam AWABWATUKIA FIFA.

Aliyekuwa mpinzani wa raisi wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter katika uchaguzi mkuu uliofanyika june mosi mwaka huu, Mohammed Bin Hammam, amelituhumu Shirikisho hilo kwa kudai linavifumbia macho vitendo vya ubaguzi wa Rangi.

Mohammed Bin Hammam ambae pia alikua raisi wa shirikisho la sojka barani Asia, amesema kasumba ya ubaguzi wa rangi imemponza na pengine angekua mzungu asingefungiwa maisha katika harakati wa kujihuisisha na masuala ya soka.

Mwanamichezo huo ambae alikumbwa na kadhia ya kutao rushwa wakati wa kufanya kampeni za kuwania kiti cha uraisi amezielekeza lawama hizo kwa viongozi wote waliohusiska na adhabu iliyomkuta miezi miwili iliyopita.

Katika tovuti ya Bin Hamman ujumbe huo wa kubaguliwa kutokana na rangi yake umemlenga mwenyekiti wa kamati ya maadili ya shirikisho la soka duniani kote FIFA, Petras Damaseb ambaye mwishoni mwa mwezi May aliwasilisha hukumu yake.

Pia ujumbe huo umeongeza kwamba endapo angekua mzungu, si Sepp Blatter wala katibu mkuu wa FIFA Jarome Valke wasingethubutu kumnyooshea kidole kwa madai ya kumkuta na kadhia ya rushwa.

Juma moja kabl ya uchaguzi mkuu wa FIFA Bin Hamman alidaiwa kuwarubuni baadhi ya wajumbe wa Carribean, kwa kuwapa mlungula ili wamchague katika uchaguzi mkuu ambao ulipangwa kufanyika June mosi mjini Zurich nchini Uswiz.

No comments:

Post a Comment