KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, September 14, 2011

Neymar da Silva Santos Júnior HAUZWI.

Raisi wa klabu ya Santos ya nchini Brazil Alvaro de Oliveira amekanusha taarifa za kufanya makubaliano ya kumuuza mshambuliaji wa klabu hiyo Neymar da Silva Santos Júnior kunako klabu ya Real Madrid ama FC Barcelona zote za nchini Hispania.

Alvaro de Oliveira amekanusha taarifa hizo, ikiwa ni siku kadhaa baada ya vyombo vya habari nchini Brazil pamoja na nchini Hispania kuripoti kwamba viongozi wa klabu hiyo wapo tayari kumuachia mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 19.

Amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote na wala hakuna kiongozi wa Santos aliekaririwa na vyombo hivyo vya habari ambavyo amedia haviitakii mema klabu yao.

Hata hivyo Alvaro de Oliveira amedai kwamba mara baada ya taarifa hizo kutoka katika vyombo vya habari alifanya mawasiliano na raisi wa Fc Barcelona Sandro Rosell pamoja na raisi wa Real Madrid Florentino Perez kwa ajili ya kuwauliza juu ya suala hilo lakini pia walikanusha vikali.

Amedai kuwa licha ya kuwauliza viongozi wa klabu hizo nguli nchini Hispania pia aliwataka kutokua na ukimya endapo litaibuka suala lingine linalomuhusu Neymar da Silva Santos Júnior na ikiwezekana wakae mezani na kulimaliza.

No comments:

Post a Comment