KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, September 17, 2011

NI VITA YA MANENO KATI YA BABA NA MTOTO.

Ligi ya nchini Uingereza itaendelea tena kesho kwa michezo kadhaa kuchezwa katika viwanja tofauti lakini mchezo mkubwa unaosubiriwa kwa hamu ni kati ya Man Utd dhidi ya Chelsea utakaounguruma Old Trafford ambapo ni nyumbani kwa Mashetani wekundu.

Tayari vita ya maneno kati ya mameneja wa klabu hizo mbili imeshaanza kutawala ambapo Sir Alex Ferguson amempiga dongo boss wa klabu ya Chelsea Andre Villas-Boas kwa kusema itakua miujiza endapo atachukua ubingwa wa nchini humo akiwa na umri wa miaka 33.

Sir Alex Ferguson ametoa dogo hilo huku akielewa fika Andre Villas-Boas ana matumaini makubwa ya kuandika historia kama hiyo ambayo haijawahi kutokea nchini Uingereza toka mfumo wa ligi kuu ulipoanzishwa February 20-1992.

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 69, ameendelea kueleza kwamba kwa umri wa meneja huyo ni shughuli kubwa kufanya kazi katika klabu kama ya Chelsea hivyo anamsikitikia kutokana na mazingira ya klabu hiyo.

Hata hivyo amedia kwamba mchezo wa kesho utakua mgumu lakini anaupa nafasi kubwa upande wa wachezaji wake ambao upo vizuri toka msimu huu ulipoanza kutokana umahiri wa kila mchezaji anaempa nafasi kikosini.

Nae meneja wa Chelsea Andre Villas-Boas amesema anamuheshimu sana Sir Alex Ferguson na katu hawezi kujifananisha nae kutokana na mafanikio makubwa aliyoyapata toka alipoaingia katika mchezo wa soka zaidi miaka 30 iliyopita.

Amesema meneja huyo ni mwenye heshima na kila mmoja katika medani ya soka anastahili kuheshimu anachokifanya, hivyo atakwenda katika mchezo wa kesho akiwa katika misingi hiyo.

Lakini kwa upande mwingine Villas-Boas, akabainisha kwamba soka ni mchezo ambao hautegemei nani mwenye heshima hivyo msema kweli nio dakika 90 ambazo zitaamua nani ataondoka na point tatu huko Old Trafford.

Katika hatua nyingine meneja huyo kutoka nchini Ureno akaendelea kusisitiza jambo la kukipanga kikosi chake kwa kusema ataendelea na mfumo kama alioutumia kabla ya mchezo wa Bayer Leverkusen ambapo kila mchezaji atajumuishwa kikosini kutokana na jitihada zake binafsi.

Michezo mingine ya ligi hiyo itakayounguruma kesho ni pamoja na;

White Hart Lane, London
Tottenham Hotspur v Liverpool

Craven Cottage, London
Fulham v Manchester City

Stadium of Light, Sunderland
Sunderland v Stoke City

No comments:

Post a Comment