KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, September 2, 2011

Nicklas Bendtner HAITAKI TENA ARSENAL.

Mshambuliaji kutoka nchini Denmark na klabu ya Arsenal Nicklas Bendtner amesema hatamani tena kurejea jijini London baada ya kujiunga na Sunderland kwa mkopo usiku wa kuamkia Septemba mosi.

Nicklas Bendtner amesema mazingira ya upatikanaji wa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha mzee Arsene Wenger ndio yanayomsukuma kufikiria kubaki moja kwa moja huko Stadium of Light na ikiwezekana kuondoka kabisa katika klabu hiyo atakapomaliza mkataba wake wa mkopo.

Amesema anaipenda sana Arsenal, kutoka na mshikamano uliopo ndani ya kikosi na angetamani kuendelea kuichezea klabu hiyo, lakini amedai umefikia wakati anahitaji kucheza kila juma kama ilivyo kwa wachezaji wengine na njia sahihi anahisi ni kuondoka Emirates Stadium.

Katika hatua nyingine kiungo mshambuliaji kutoka Jamuhuri ya watu wa Korea aliesajiliwa na washika bunduki wa Ashburton Grove Arsenal Park Chu-young ametuma salamu kwa mashabiki wa klabu hiyo ya jijini London baada ya kupachika mabao matatu kati ya mabao sita yaliyo ididimiza timu ya taifa ya Lebanon katika mchezo wa kuwani nafasi ya kucheza fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 ukanda wa barani Asia.

Park Chu-young aliesajiliwa na Arsenal akitokea AS Monaco ya nchini Ufaransa kwa ada ya uhamisho wa paund million 3, alionekana kuwa mwiba mkali wa safu ya ulinzi wa timu ya taifa ya Lebanon kila mara na wakati mwingine alitengeneza nafasi ya upatikanaji wa mabao mengine.

Alipohojiwa na vyombo vya habari mara baada ya mtanange huo kumalizika, alisema huu ni mwanzo wake mzuri na anaamini hatua ya kufunga mabao matatu katika mchezo huo kutamsaidia kujiamini na kuanza maisha tofauti akiwa na klabu mpya.

Kwa upande wa kiungo kutoka nchini Hispania Mikel Arteta nae amzungumzia hatua ya uhamisho wake katika dakika za mwisho akitoka Everton kuelekea kaskazini mwa jiji la London yalipo makao makuu ya klabu ya Arsenal.

Amesema ndoto zake za kuichezea klabu hiyo kubwa zimetimia pamoja na kucheza katika ligi ya mabingwa barani ulaya, huku akiwashukuru mashabiki na uongozi wa klabu ya everton kwa ushirikiano waliompa toka alipojiunga nao mwaka 2005 akitokea Real Sociedad.

Wachezaji wengine waliosajiliwa na Arsenal mara baada ya kisago cha mabao manane kwa mawili kilichotolewa na Man utd mwishoni mwa juma lililopita ni Mikael Arteta, Per Mertesacker, Yossi Benayoun pamoja na André Santos.

No comments:

Post a Comment