KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, September 15, 2011

NINACHUKIWA KWA SABABU MIMI TAJIRI, MZURI NA UWEZO WA UWANJANI - CRISTIANO RONALDO.

Mchezaji ghali duniani Cristiano Ronaldo amesema mara kadhaa anapopata mapokezi mabaya kutoka kwa mashabiki wa klabu pinzani huwa anatambua hatua hiyo inatokana na utajiri wake, sura yake nzuri na umahiri wake anapokua uwanjani.

Cristiano Ronaldo ametoa mtazamo huo kufutia mapokezi mabaya aliyoyapata kwa mashabiki wa klabu ya Dinamo Zagreb ambayo jana walikutana nayo katika michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya.

Katika mchezo huo Cristiano Ronaldo, alipata wakati mgumu wa kuzomewa na mashabiki wa Dinamo Zagreb kila alipoguza mpira na kila alipochezewa rafu hatua ambayo amedai ilimkera yeye kama mchezaji ambae hana kosa zaidi ya kuitumikia klabu yake.

Hata hivyo amedai kwamba mbali na mashabiki wa Dinamo Zagreb, pia hupata mapokezi mabaya kila anapokua na Real Madrid nje ya nchi ya Hispania ambapo mashabiki humzomea na kumuambia wazi wazi huwezi kufanana na Messi hata kidogo.

Katika hatua nyingine kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26, amesema mbali na mapokezo mabaya aliyoyapata, yeye binafsi pamoja na wachezaji wengine wa Real Madrid wamefurahishwa na matokeo ya bao moja kwa sifuri ambayo yamewapa point tatu muhimu katika msimamo wa kundi la nne.

Bao hilo pekee la The Galacticos lilipachikwa wavuni katika dakika ya 53 na winga kutoka nchini Argentina Angel di Maria.

No comments:

Post a Comment