KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, September 6, 2011

Queens Park Rangers WAKANUSHA UVUMI WA David Beckham.

Uongozi wa klabu ya Queens Park Rangers umekanusha taarifa za kuwa mbioni kumrejesha nyumbani kiungo kutoka nchini Uingereza David Beckham ambae kwa sasa anaitumikia Los Angels Galax ya nchini Marekani.

Queens Park Rangers wamekanusha taarifa hizo zikiwa zimepita siku kadhaa baada ya kuhusishwa na utaratibu huo ambao uliwashutua wengi ulimwenguni kote kutokana na umahiri wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 36.

Makamu mwenyekiti wa klabu hiyo iliyorejea katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza msimu huu baada ya kushuka mwaka 1996, Amit Bhatia amesema taarifa za kutaka kumsajili David Beckham si za kweli lakini zimewafurahisha pale walipoziona na kuzisikia kupitia radio na televisheni.

Amesema ni jambo zuri kuwa na mchezaji mwenye uzoefu katika kikosi kama cha Queens Park Rangers, lakini kwa sasa wanatazama uwezekano huo na si kwa kukamilisha matakwa ya watu kupitia fununu za kumsajili David Beckham.

David Beckham, kwa sasa bado ana mkataba wa kuitumilia Los Angles Galax hadi mwezi Novemba mwaka huu, na bado haijafahamika kama atasaini mkataba mpya na klabu hiyo ama la.

No comments:

Post a Comment