KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, September 13, 2011

Rafael van der Vaart AKASIRISHWA NA SPURS.

Kiungo mshambuliaji kutoka nchini Uholanzi Rafael van der Vaart amesema amekasirishwa na kitendo cha jina lake kuondolewa katika usajili wa wachezaji watakaocheza michuano ya ligi ya barani ulaya msimu huu.

Rafael van der Vaart amesema amekasirishwa na kitendo hicho kufuatia benchi la ufundi kufanya maamuzi hayo bila kumshirikisha yeye kama mchezaji hatua ambayo kwake ameichukuliwa kama amedharauliwa.

Amesema kila mmoja ndani ya klabu hiyo anatakiwa kuheshimiwa kutokana na mchango anaoutoa katika kikosi, hivyo jambo hilo litaendelea kumuuma tena sana kutokana na uhalisia wa ndoto zake za kutaka kucheza katika michuano ya barani ulaya.

Hata hivyo sababu kubwa ya benchi la ufundi la Spurs la kukata jina la kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28, ni kutokana na majeraha ambayo yamekua yakimuandama mara kwa mara na hivi sasa hali hiyo inamsumbua toka katika mchezo wa ligi dhidi ya Man city.

Kwa mantiki hiyo sasa meneja wa Spurs Harry Redknapp amekusudia kuwatumia wachezaji chipukizi badala ya kiungo huyo kama Harry Kane, Tom Carroll na Jake Livermore katika michuano ya ligi ya barani ulaya ambapo juma hili watacheza dhidi ya klabu ya PAOK Salonika toka nchini Ugiriki.

No comments:

Post a Comment