KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, September 2, 2011

Rafael van der Vaart NJE YA UWANJA KWA MAJUMA SITA.

Juma moja baada ya kuangushiwa kipondo cha mabao matano kwa moja kutoka kwa Man City, Tottenham Hotspurs wameendelea kupata pigo kufuatia kiungo wao kutoka nchini Uholanzi Rafael van der Vaart kuamuriwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa majuma sita yajayo.

Rafael van der Vaart, ameamriwa kuwa nje ya uwanja kwa kipindi hicho kufuatia jeraha la nyama za paja alilolipata mwishoni mwa juma lililopita katika mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza mwishoni mwa juma lililopita.

Taarifa zilizotolewa na jopo la madaktari wa Spurs zimeeleza kuwa vipimo alivyofanyiwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28, vimeonyesha kwamba Rafael van der Vaart ameumia kwa kiasi kikubwa na sasa inamlazimu kutulia ili aweze kurejea katika hali yake ya kawaida.

Kwa mantiki hiyo sasa Rafael van der Vaart, ataanza kuonekana tena uwanjani kati kati ya mwezi wa kumi, endapo matarajio ya madaktari yatafanikiwa na endapo itakua kinyume na hapo huenda muda wa kuwa nje ya uwanja ukaongezeka zaidi.

Atakapo kuwa nje ya uwanja, kiungo huyo atakosa michezo ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza dhidi ya Wolverhampton Wanderers, Liverpool, stoke city, wigan Athletics pamoja na Arsenal utakaopigwa October 2.

No comments:

Post a Comment