KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, September 8, 2011

Roberto Martinez ATOA MSIMAMO TOFAUTI.


Baada ya kupisha juma la michezo ya kimataifa ulimwenguni kote, meneja wa Wigan Atheltics Roberto Martinez amesema anaamini wachezaji wake wamerejea wakiwa vizuri kabla ya kupambana katika mchezo wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Man City.

Roberto Martinez yeye binafsi anaamini juma la michezo ya kimataifa limewajenga kiushindani wachezaji wake ambao walipata ushindi wa mabao mawili kwa sifuri katika mchezo uliopita wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza dhidi ya klabu iliyopanda daraja msimu huu QPR.

Amesema huenda yeye akawa meneja mwenye hisia tofauti hasa ikizingatiwa mameneja wengine wa vilabu huwa wanapiga sana vita tarehe za michezo ya kimataifa kwa kuamini huenda wachezaji wao watakaporejea watakua majeruhi lakini kwake ni kinyume.

Katika hatau nyingine Roberto Martinez ambae ni raia wa nchini Hispania akasifia usajili alioufanya katika dakika za lala salama kwa kumpata mshambuliaji kutoka nchini Scotland na klabu ya Celtic Shaun Maloney, winga kutoka nchini Hispania na klabu ya Almeria Albert Crusat pamoja na beki kutoka nchini Uholanzi na klabu ya Chelsea aliemsajili kwa mkopo wa muda mrefu Patrick van Aanholt.

Kama itakumbukwa vyema msimu uliopita Roberto Martinez alijitahidi na kufanikiwa kuibakisha klabu ya Wigan katika michuano wa ligi kuu, baada ya kuwepo katika ukanda wa kushuka daraja hadi mwishoni mwa ligi.

No comments:

Post a Comment