KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, September 15, 2011

SAMAHANI BABA - Roberto Mancini.

Meneja wa Man City Roberto Mancini usiku wa kuamkia hii leo alilazimika kumtaka radhi baba yake mzazi Aldo Mancini aliefunga safari kutoka nchini Italia hadi mjini Manchester kwa ajili ya kutazama mchezo wa ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya Società Sportiva Calcio Napoli.

Roberto Mancini amelazimika kufanya hivyo kufutia mambo kumuendea kombo huko Etihad Stadium ambapo mashabiki walishuhudia kikosi cha Man city kikisawazisha bao kupitia kwa Aleksandar Kolarov baada ya mshambuliaji kutoka nchini Uruguay Edson Cavan kuifungia SSC Napoli bao la kuongoza.

Amesema hana budi kumtaka radhi baba yake mzazi kwani aliamini mzee huyo alifunga safari ya kwenda kuitazama kazi yake huku akimini huenda wangeibuka na ushindi katika mchezo huo wa kundi la kwanza.

Hata hivyo Mancini amesema kwamba baba yake mzazi ataendelea kuwepo nchini Uingereza hadi mwishoni mwa juma hili, kwa ajili ya kutazama mchezo wa ligi kuu ambapo Man city watasafiri hadi jijini London kwenda kucheza na Fulham huko Craven Cottage.

Katika hatua nyingine meneja huyo kutoka nchini Italia ametetea matokeo yaliyopatikana mbele ya Società Sportiva Calcio Napoli kwa kusema si matokeo mabaya kwao na anahisi mwenendo uliwaendea kombo kutokana na ugeni wa michuano hiyo ambapo Man City wanashiriki baada ya miaka kadhaa kupitia.

Amesema kikosi chake kilionyesha uwezo mkubwa katika kipindi cha kwanza lakini katika kipindi cha pili mambo yaliwaendelea tofauti na pengine hatua hiyo anadhani ilitokana na ushawishi wa wachezaji wake kusaka bao la kusawazisha.

Roberto Mancini hakuishia hapo bali aliendelea kutanabai kwamba kuanza kwao kwa matokeo ya sare, kuna wajengea nafasi nyingine ya kutengeneza mipango ya kusaka ushindi katika mchezo ujao ambao utawakutanisha na Bayern Munich huko nchini Ujerumani Sept 27.

No comments:

Post a Comment