KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, September 14, 2011

SARE SIO MBAYA KWETU - PAT RICE.

Sare ya bao moja kwa moja ambayo ilishuhudia washika bunduki wa Ashburton Grove wakiondoka nchini humo na point moja dhidi ya mabingwa wa Bundesliga Borusia Dotmund imezungumzwa vizuri na meneja msaidizi wa Arsenal Pat Rice ambae alishika pahala pa bosi wake Arsene Wenger aliekua jukwaani.

Pat Rice amesema si matokeo mabaya kwa kikosi chake kutokana na mtazamo wa mchezo ulivyokua, hivyo ameahidi kujipanga zaidi kwa ajili ya michezo mingine ya kundi la sita ambapo Arsenal watakutana na Olympiacos Sept 28 katika uwanja wa nyumbani wa Emirates.

Amesema katika mchezo huo wa jana wapinzani wao walionyesha uwezo mkubwa wa kulishambulia lango lao mara kwa mara lakini umakini wa safu ya ulinzi wa The Gunners ulisaidia kuokoa purukushani za Borussia Dortmund ambazo hata hivyo zilizaa matunda katika dakika ya 88 kupitia kwa kiungo mshambuliaji kutoka nchini Croatia Ivan Perišić.

Katika hatua nyingine Pat Rice amesema alikua hana amani ya kutosha alipokua katika benchi la klabu ya Arsenal na alikasirishwa na kila dakika ya mchezo huo ilivyokua ikipotea kutokana na upungufu wa kutokuwepo kwa bosi wake, lakini amewashukuru wachezaji kwa kuienzi kazi yake.

Nae mfungaji wa bao la Arsenal ambae pia ni nahodha Robin Van Parsie amesema hawana budi kuyapokea kwa mikono miwili matokeo hayo, kutokana na mazingira ya ugenini yaliyokua yamewazunguuka.

Amesema Borussia Dortmund ni klabu nzuri ambayo imekua ikisaidiwa sana na mashabiki wake wanapokua nyumbani hivyo walijitahidi kadri ya uwezo wao.

No comments:

Post a Comment