KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, September 6, 2011

Steed Malbranque APINGA VIKALI KUSTAHAFU SOKA.

Kiungo kutoka nchini humo Steed Malbranque amekanusha vikali taarifa za kustahafu soka ambazo ziliripotiwa na vyombo mbali mbali huko barani ulaya mwishoni mwa juma lililopita kwa kisingizio cha kuuguliwa na mwanae.

Steed Malbranque ambae aliwahi kuitumikia klabu ya Fulham, Tottenham pamoja na Sunderland zote za nchini Uingereza amekanusha taarifa hizo kupitai kwa wakala wake, Sebastien Boisseau ambapo amesema hakuna ukweli wowote juu ya suala hilo la kutundika daluga kwa kisingizio cha kuuguliwa na mwanae wa kiume.

Amesema kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa katika vyombo vya habari ambazo zilidai kwamba ameamua kuacha soka kufuatia mwanae wa kiume kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani, si kweli kwani katika maisha yake hakuwahi kupata mtoto wa kiume.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31, pia akaanisha wazi kwamba hata kama taarifa hizo zingeripotiwa kuna mtu ndani ya familia yao ana ugionjwa wa kansa, bado zisingekua na ukweli, kwani hakuna mtu yoyote alie na ukaribu nae anasumbuliwa na ugonjwa huo.

Katika hatua nyingine Steed Malbranque, amesitisha mkataba wake na klabu ya St Etienne ya nchini Ufaransa kwa makubaliano binafsi na uongoizi wa klabu hiyo ambayo hakutaka yawekwe hadharani.

Steed Malbranque amesitisha mkataba wake ikiwa ni miezi miwili tu baada ya kujiunga na klabu hiyo akitokea kwenye klabu ya Sunderland ya nchini Uingereza.

No comments:

Post a Comment