KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, September 3, 2011

Steed Malbranque ATUNDIKA DALUGA.

Kiungo mshambuliaji kutoka nchini humo Steed Malbranque ametangaza kustahafu soka ikiwa ni siku chache baada ya kuanza kuitumikia St Etienne akitokea Sunderland.

Steed Malbranque amefikia maamuzi hayo huku akiwa amecheza mchezo mmoja akiwa na klabu ya St Etienne tena akitumiwa kama mchezaji wa akiba katika mchezo wa ligi daraja la kwanza nchini Ufaransa dhidi ya Sochaux.

Sababu kubwa iliyomfanya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 kuamua kutundika daluga ni matatizo ya kiafya yanayomuandama mtoto wake wa kiume anaesumbuliwa na ugonjwa wa sarakati hali ambayo inamalazimu kuwa na mtu wa karibu wa kuamuangaluia.

Steed Malbranque alizaliwa nchini Ubelgiji na alipofikisha umri wa miaka 12 alipelekwa katika shule za mchezo wa soka nchini Ufaransa hatua ambayo ilimlazimu kubadilisha uraia na kufikia wakati aliweza kuitumikia timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 21 ya nchi hiyo lakini hakubahatika kuitwa katika kikosi cha wakubwa.

Katika upande wa soka la kulipwa Steed Malbranque alianza kuitumikia klabu ya Olympic Lyonais ya nchini Ufaransa, kisha alielekea nchini Uingereza na akiwa huko alizitumikia klabu kama Fulham Tottenham Hotspur pamoja na Sunderland kabla ya kurejea nchini Ufaransa kujiunga na Saint-√Čtienne miezi miwili iliyopita.

No comments:

Post a Comment