KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, September 6, 2011

Thomas Vermaelen NJE MWEZI MMOJA.

Siku moja baada ya kutolewa taariafa za kuwa nje ya uwanja kwa kiungo mkabaji wa nchini Uingereza Jack Wilshere, Washika bunduki wa Ashaburton Grove Arsenal wamepata pigo lingine kufuatia beki wao wa kati kutoka nchini Ubelgiji, Thomas Vermaelen kutarajia kuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha mwezi mmoja ujao.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 25, anatarajia kuwa nje ya uwanja kwa kipindi hicho kufuatia kufanyia upasuaji wa kisigino, akiwa mjini Stockholm nchini Sweden usiku wa kuamkia hii leo.

Thomas Vermaelen alipatwa na maswahibu ya kuumia kisigino akiwa katika mchezo wa pili wa kuwania nafasi ya kucheza hatua ya makundi la ligi ya mabingwa barani Ulaya, ambapo Arsenal walichomoza na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Udanise, na kupata ushindi wa jumla wa mabao matatu kwa moja.

Kufuatua hatua hiyo beki huyo hakuwepo kikosini katika mchezo wa ligi uliopita ambapo Arsenal walikubali kisago cha mabao manane kwa mawili, na pia alitangaza kujiondoa katika timu ya taifa ya Ubelgiji ambayo imerejea mstuni kusaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya barani ulaya za mwaka 2012.

Kama itakumbukwa vyema, msimu uliopita Thomas Vermaelen hakucheza kwa kipindi cha miezi kadhaa, kutokana na jeraha la kisigino lililokua likimuandama kushindwa kupona kwa wakati muafaka.

No comments:

Post a Comment