KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, September 12, 2011

TORRES KUKAA BENCHI KATIKA GAME YA KESHO.

Mshambuliaji kutoka nchini Hispania Fernando Torres huenda akaachwa katika kikosi cha Chelsea kitakachocheza kesho katika mchezo wa ufunguzi wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Bayer-Leverkusen.

Fernando Torres yupo katika hati hati ya ya kuenguliwa katika mchezo huo kufuatia meneja wa Chelsea Andre Villas-Boas kufikiria kumchezesha mshambuliaji kutoka nchini Uingereza Daniel Sturridge ambae mwishoni mwa juma lililopita aliifungia The Blues bao la pili dhidi ya Sunderland.

Andre Villas-Boas amesema matarajio yake ni kuanza vyema ligi ya mabingwa barani Ulaya hivyo atahakikisha anapanga kikosi ambacho kitafikia malengo hayo mazuri, hatua ambayo inaonekana haiwezi kumpa nafasi Torres kutokana na mwenendo wake toka alipohamia klabuni hapo kusua sua.

Amesema kwa ujumla kikosi chake ni kizuri lakini uzuri unatengenezwa na wachezaji wenye mipango ya kuhakikisha Chelsea inasonga mbele katika michuano yote wanayoshiriki na watakayoshiriki msimu huu.

Endapo Torres ataachwa katika kikosi cha kesho, litakua pigo kubwa kwake kutokana na mwishoni mwa juma lililopita alifanyiwa hivyo katika mchezo dhidi ya Sunderland huku akitumika kama mchezaji wa akiba.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, toka alipoelekea Chelsea amefanikiwa kufunga bao moja mpaka sasa, hatua Ambayo imezua minong’ono kwa mashabiki wake pamoja na wale wa The Blues kwa kudai bado hajalipa fadhila ya kitita cha paund million 50 kilichotumuka kumsajili akitokea Liverpool mwezi januari mwaka huu.

No comments:

Post a Comment