KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, September 8, 2011

UEFA KUKOMAA NA WAVUNJA SHERIA.


Shirikisho la soka barani ulaya UEFA limesema litaanza kuviadhibu vilabu vitakashindwa kuheshimu kanuni za usajili kwa kufuata taratibu za kifedha kwa mujibu wa kanuni zilizopitishwa na shirikisho hilo kuhusu matumizi ya fedha za klabu.

Adhabu kali kwa klabu zitakazokwenda kinyume na sheria hiyo ni kuondolewa katika michuano ilio chini ya UEFA lakini pia uongozi wa shirikisho hilo umeshatoa taarifa kwa umoja wa vilabu vya barani Ulaya European Club Association (ECA) huenda ukatoa adhabu zaidi ya hiyo.

Naye mkurugenzi mtendaji wa klabu ya Inter Milan ya nchini Italia Ernesto Paolillo amesema klabu inayotumia fedha zaidi katika usajili na kukiuka masharti ya UEFA inatakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria zaidi kuliko kimichezo.

Amesema klabu nguli za barani ulaya, zinatakiwa kuadhibiwa mara moja endapo zitakiuka kanuni zilizowekwa, ili iwe fundisho kwa klabu nyingine zinazotarajia kufanya usajili kinyuma na matakwa ya UEFA.

No comments:

Post a Comment