KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, September 3, 2011

UHOLANZI WAFANYA KUFURU UWANJANI.

Timu ya taifa ya Uholanzi, imevunja rikodi yake yenyewe baada ya kuitandika timu ya taifa ya San Marino mabao 11 kwa sifuri katika mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka 2012 zitakazochezwa nchini Poland pamoja na Ukraine.

Timu ya taifa ya Uholanzi imeweka rekodi mpya huku mashabiki wengi wa soka ulimwenguni wakikumbuka rekodi iliyowekwa mwaka 1912 na timu hiyo pale ilipotoa kichapo cha mabao tisa kwa sifuri dhidi ya timu ya taifa Finland pamoja na timu ya taifa ya Norway iliweza kupokea kisago kama hicho mwaka 1972.

Ushindi huo wa mabao 11 kwa sifuri dhidi ya San Marino umepatikana huku timu ya taifa ya Uholanzi ikicheza nyumbani na sasa unaifanya nchi hiyo kuongoza kundi la sita kwa kufikisha point 21 ambazo zinatengeneza tofauti ya point 6 dhidi ya timu ya taifa ya Sweden pamoja na timu ya taifa ya Hungary.

Wafungaji wa mabao hayo kumi na moja ni mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Robin Van Persie alieingia nyavuni mara nne, kiungo wa Inter Milan Wesley Sneijder na mshambuliaji wa Schalke 04 Klaas Jan Huntelaar wote wameingia nyavuni mara mbili kila mmoja, beki wa Everton John Heitinga, mshambuliaji wa Liverpool Dirk Kuyt pamoja na mshambuliaji wa PSV Eindhovein Georginio Wijnaldum wameingia nyavuni mara moja kila mmoja.

No comments:

Post a Comment