KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, September 10, 2011

VIUNGO WOTE WA CHELSEA WAZEE - Fernando Torres.

Mshambuliaji kutoka nchini Hispania Fernando Torres ametoa sababu za kushindwa kupachika mabao kama alivyokua akitarajiwa na mashabiki wa Chelsea toka alipojiunga na klabu hiyo mwezi Januri mwaka huu akitokea Liverpool.

Fernando Torres ambae mpaka sasa ameshaifungia Chelsea bao moja katika ligi pamoja na michuano ya kimataifa amesema klabu hiyo, imekua na viungo wazito ambao wanashindwa kumuwezesha kufunga kama alivyokua huko Anfield.

Amesema alipohamia klabuni hapo alitambua tatizo hilo na alijitahidi kuizoea hali hiyo siku hadi siku lakini mambo yameendelea kumuendea kombo mpaka hii leo ambapo amekiri kutambua kuwa na deni la kuwafurahisha mashabiki wa The Blues.

Hata hivyo amedia kwamba uzito wa viungo wa klabu hiyo unasababishwa na umri mkubwa walionao na ndio maana meneja mpya Andre Villas Boas ameamua kumsajili kiungo Juan Mata ambae anaamini atamuwezesha kurejesha makali yake.

Kauli hiyo ya Fernando Torres imekuja baada ya saa 24 kupita ambazo zilishuhudia Andre Villas Boas akizungumzia uaminifu wake dhidi ya mshambuliaji huyo kwa kusema mazuri yanakuja kutoka kwake.

Huenda mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, amepata nguvu ya kutoa sababu za kushindwa kufunga, kama alivyokua anatarajiwa kutokana na kutumainiwa na meneja wa Chelsea ambae msimu uliopita aliiwezesha Fc Porto kutwaa ubingwa wa nchini Ureno pamoja na ligi ya barani Ulaya.

No comments:

Post a Comment